Thursday, March 28, 2013

Wapenzi wa mashairi kazi kwenu

" TUTABAKI MARAFIKI"
Mimi kuongea nawe, usidhani nakutaka
Usijepata kiwewe, na kichwa kikafutuka
Ninaomba uelewe, uyaondoshe mashaka
Siwezi kuwa na wewe, tutabaki marafiki

Nikweli nilikupenda, pendo lisilo mashaka
Popote nilipokwenda, kukuwacha sikutaka
Lakini ukaniponda, kaniona takataka
siwezi kuwa na wewe, tutabaki marafiki
Bofya hapa kusoma zaidi