Sunday, April 13, 2014

AJALI - MAKAMU WA RAIS DK. BILAL, KOVA, MKUU WA MKOA WA DAR NA DK. MAGUFULI WAPATA AJALI YA HELIKOPTA (picha)


Kutokana na mvua kubwa kunyesha jiji Dar es salaam na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundo mbinu, Makamu wa Raisi D.K Mohammed Gharib Bilal, Dk.Jaohn Magufuli, mkuu wa mkoa wa Dar, Meck Sadiki na Afande Kova, walikuwa katika mishemishe za kwenda kutembelea maeneo mbalimbali yaliyoharibika. 




Lakini kwa bahati mbaya wakati Helkopta waliyokuwa wanaitumia kama usafiri, ilidondoka na kuwaka moto mara tu ilipokuwa inaanza kupaa. Hata hivyo katika ajali hiyo watu wote walinusurika na kutoka wakiwa wazima. 

Mungu ibariki Tanzania - Mungu wabariki viongozi wa Tanzania.