Saturday, April 12, 2014

MBARONI KWA KOSA LA KUTUPIA PICHA ZA UCHI ZA EX-GIRLFRIEND WAKE MTANDAONI

Kijana mwenye umri wa miaka 26 amejikuta akitiwa Mabaroni kwa kosa la kuchukua picha za mpenzi wake (ex girlfriend) na kuzimimina katika mtandao wa Facefacebook. 

Binti aliyefanyiwa uchafu huwo na kijana huyo aliyefahamika kwa jina la David Dickson amedai kuwa alichukua uamuzi wa kuachana na mwanaume huyo kwasababu alitoka kimapenzi na rafiki yake wa karibu. Alisema kuwa baada ya kuamua kuchukua uamuzi wa kuachana naye, kijana huyo akaona atumie nafasi kuonesha umwamba wake baada ya kumbembeleza warudiane pasipo mafanikio.

Kwa mujibu wa mahakama, inasemekana kuwa picha za utupu zilizowekwa na mwanaume huyo kwa namna moja ama nyingine zinatumiwa na watu wengine na kuzidi kuzieneza. Kwa maantiki hiyo, mahakama inatoa onyo kwa watu wenye tabia kama hiyo kwasababu ni udhalilishaji wa kijinsia na inasababisha wanaofanyiwa vitendo kama hivyo kuathirika kisaikolojia.

Kwa mujibu wa wakili wa kesi hii, mtuhumiwa na mlalamikaji ni wapenzi kwa muda wa miaka miwili. Lakini kutokana na kitendo cha mtuhumiwa kufanya mapenzi na rafiki wa mlalamikaji amabye alikuwa ni mpenzi wake, Uhusiano huo ukavunjika.

Wakila alisema kuwa mlalamika alipigiwa simu na rafiki yake akimtaka afungue mtandao wa Faceboo na WatsAp ili kuangalia kilichokuwa kinaendelea.

Mlalamikaji alifanya kama rafiki yake huyo alivyomsihi. Alijikuta akibaki mdomo wazi na kufadhaika baada ya kukuta picha zake za utupu zikipepea mtandaoni. Mlalamikaji alipompigia simu David na kumuuliza juu ya kile kile kilichotokea, David alikiri kuhusika na tukio lile huku akidai kuwa aliamua kufanya vile ili kumchafua asiweze kuwa na mwanaume mwengine zaidi yake yeye.

Malamikaji alikwenda kutoa taarifa hizo katika kituo cha polisi, na mtuhumiwa akatiwa mbaroni mara moja.

Kwa mujibu wa wakili, anaeleza kuwa inaonekana mtuhumiwa David anampenda sana mpenzi wake, na baada ya kuachwa hakuwa anaelewa kitu ambacho kingetokea mbeleni.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA CHINI