Friday, May 23, 2014

AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA KWA KOSA LA KUMBAKA MTOTO NDANI YA MSIKITI

Kutokana na tukio la kusikitisha lilotokea hivi karibuni mwezi Mei 8, mwaka huu saa nne asubuhi, la mwanaume mmoja kumbaka mtoto wa kike ndani ya msikiti wa Kawawa, Liwale huko Lindi. Mahakama ya wilaya hiyo imemhukumu mtuhumiwa huyo kifungo cha miaka 30 jela



Mahakama ya Wilaya hiyo ya Liwale chini ya Hakimu Mfawidhi, Eric Ruhumbiza,  imemtia hatiani mshtakiwa kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 11, chini ya vifungu namba 130 na 131 vya sheria ya makosa ya Kujamiiana (Sospa) ya mwaka 1998.


Hakimu wa mahakama hiyo amesema kuwa, mahakama imetoa hukumu hiyo baada ya kuridhishwa na ushahidi uliowasilishwa upande wa mlalamikaji mahakamani hapo. 


Shahidi namba tano ambaye ni mtoto aliyefanyiwa unyama huwo, ameiridhisha mahakama hiyo kutokana na maelezo aliyoyatoa kuhusu maumbile na viungo vya siri vya mtuhumiwa.

Mwendesha Mashata ameeleza kuwa, kabla mshtakiwa kufanya tukio hilo, alimuingiza mtoto huyo msikitini, sehemu ambayo wanawake wanaswalia, alimlaza chini na kumvua nguo huku akimfunika kwa kanga usoni.


Aliendelea kueleza kuwa mshtakiwa kabla ya kumbaka mtoto huyo alimuwekea kitabu kitukufu cha Quran kichwani na kumwambia kuwa kwa aya anayomsomea, akimweleza mtu kitu atakachomyanyia atageuka kipofu.


Jambo hilo lilifahamika baada ya mfanya biashara katika eneo la shule iliyopo karibu na msikiti huwo, kutilia shaka nyendo za mwalimu huyo wa dini kuingia kwenye msikiti upande wa wanawake na kutoka kila mara kuchungulia nje.










__________________________________________________________________________________________________