Thursday, May 22, 2014

VIJANA WANAOJIITA PANYA-ROAD WAFUNGA MTAA BAADA YA MWENZAO KUUAWA KWA TUHUMA ZA WIZI



Vijana wanaotambulika kwa jina la Panya road maeneo ya Kigogo wameanzisha kitimtim Jana jumatano baada ya kijana mwenzao, Rama (dogo Rama) kuuawa na wananchi wenye hasira kali kwa tuhuma za wizi maeneo ya Sambusa.

Vijana hao wenye umri kati ya 12, 13, na 14, wameanzisha vurugu hizo jana wakati watu walipokuwa wanaelekea kwenye mazishi ya kijana mwenzao aliyeuawa. Kwa mujibu wa wananchi waliokuwa wanatoa maelezo yao kwenye kipindi cha Hekaheka redio Clouse FM, wanaeleza kuwa vijana hao walikuwa wanawaibia watu njiani wakiwemo waliokuwa wanakwenda kwenye mazishi na hata waliokuwa wanapita njia.

Baada ya mazishi vijana hao walifunga mtaa wa Sambusa kwa kufanya vurugu ikiwemo kuharibu mali za watu pamoja na kuwapiga watu wote waliokuwa wanaonekana mtaani hapo. Vurugu hizo ziliendelea hadi walipofika askari polisi na kuwatuliwa vijana hao.

Kwa taarifa na tetesi zinazosambaa wakati huu ni kwamba vijana hao (Panya road) wapo Tabata wanajipanga kwaajili ya kurudi tena mtaani kuendeleza mashambulizi.