Sunday, May 11, 2014

WAFANYAKAZI ZAIDI YA 150 WA KIWANDA CHA KUTENGENEZA VIBERITI MJINI MOSHI KILIO CHA MBWA MDOMO JUU

Matches

Kufuatia mkasa uliotokea siku chache zilizopita za kiwanda cha viberiti cha KIBO MATCH pamoja na kiwanda cha kutengeneza karatasi cha KIBO PAPER ambavyo vipo mijini Moshi mkoani Kilimanjaro kufungwa, wananchi  (wafanyakazi) zaidi ya 150 wamebakia katika wakati mgumu sana kwa kukosa ajira.


Viwanda hivyo vyote viwili vilifungwa baada ya mmiliki wake kushindwa kuviendesha kwa madai ya kuwa Vinajiendesha kwa hasara. 

Mmiliki wa viwanda hivyo ambaye ni raia wa Nigeria ameahidi kuwalipa mafao yao wafanyakazi wote. Na viwanda hivyo vitabakia vimefungwa hadi pale vitakapopatan muwekezaji mwingine.