Friday, June 26, 2015

BREAKING NEWS!! Majambazi Yavamia Benki ya NMB na Kupora Pesa Kisha Kumuua Mlinzi

Watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamevamia Benki ya NMB tawi la Mkuranga mkoani Pwani na Kupora fedha kisha kumuua Askari Mmoja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jafary Mohamed ameuthibitishia mtandao huu kutokea kwa tukio hilo na kwamba kwa sasa yupo njiani kuelekea eneo la tukio.

"Taarifa hizo nimezipata kuwa watu hao wanaodhaniwa kuwa majambazi kuvamia Benki ya NMB, Mkuranga na kupora fedha ambazo kiasi chake bado hakijafahamika kisha kumuua askari mmoja aliyekuwa nje ya uzio wa eneo hilo la benki ambaye hakuwa kazini ila walinzi wote wa benki wapo salama na silaha zao hazijachukiliwa. Kwa sasa nipo njiani kuelekea eneo la tukio kupata taarifa zaidi." Alisema Kamanda huyo.