Thursday, June 18, 2015

Watu 38 Wavamiwa Vijijini na kuuawa. BOFYA HAPA>>

Wapiganaji wa kundi la Boko Haram kutoka Nigeria wameua watu 38 katika shambulio katika vijiji viwili kusini mwa Niger.


Mbunge wa eneo hilo, Bullu Mammadu, ameiambia BBC kuwa wanawake na watoto walikuwa miongoni mwa wale waliopigwa risasi na kuuawa.

Alisema wapiganaji hao walivishambulia vijiji vya Ungumawo na Lamina Jumatano usiku na kuchoma nyumba nyingi.

Niger ni miongoni mwa mataifa yaliobuni kikosi cha kimataifa cha kukabiliana na wapiganaji hao katika eneo la magharibi mwa Afrika. 
 Chanzo: BBC