Wednesday, July 1, 2015

Basi Lingine la Abiria Lagonga treni na kusababisha Vifo na Majeruhi. MKASA MZIMA BOFYA HAPA>>

Watu watano wamepoteza maisha huku wengine 24 wakijeruhiwa baada ya basi la abiria kuligonga Treni lililokuwa linatoka Morogoro - Dodoma jana asubuhi katika eneo la Kibaoni, wilayani Kilosa mkoani morogoro.




Basi lililohusika katika ajali hiyo ni aina ya Isuzu Coaster lenye namba za usajili T837 CTM linalomilikiwa na Feisal A. Khuwel wa wilayani Kilosa.

 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa ajali hiyo imetokea jana majira ya saa 1 asubuhi na imetokana na uzembe wa dereva wa basi.



Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wiaya Kilosa, Dickson Masale amethibitisha kupokea miili ya watu watano akiwemo dereva wa basi pamoja na majeruhi 24.