Mh.Lowassa alie wasili
kisiwani Pemba na kusindikizwa na vijana kwa Pikipiki Vespa na Magari hadi hapa
kiwanja cha kibirinzi ambapo mkutano wa kampeni ulifanyika na kuwataka
wananchi wa Pemba kumkataa mgombea anae tishia amani na utulivu
kwani ndio itakayo weza kusaidia kufikisha malengo ya kuleta mageuzi ya kweli
katika nyanja zote za maendeleo na kuahidi kuwa ataimarisha Hospitali
kila wilaya kwakuweka vifaa vya kisasa.
Mh .LowasSa amesesisitiza kuwa
endapo atakuwa rais wa Tanzania atahakikisha anabadilisha mitaala ya elimu kuwa
ya kisasa ilikuliletea maendeleo ya haraka taifa la Tanzania.
Mapema mgombea mwenza wa rais
wa jamhuri ya mungano wa Tanzania kupitia umoja wa katiba ya
wananchi UKAWA Mh.Juma Duni Haji amewataka wazanzibar kushirikiana ilikufanya
mabadiliko kwa amani na utulivu nae mgombea urais wa Zanzibar kupitia
chama cha wananchi CUF Malim Seif Sharifu hamadi ameendelea kussisitiza kuwa
chama chake cha wananchi CUF hakina mpango wa kufanya vurugu kama
inavyo daiwa.
Chanzo: ITV