Chanzo chetu kimetembelea baadhi ya vituo katika
kata za Chiungtwa, Namalenga, na Lulindi na kukuta sehemu kubwa ya vituo havina
watu lakini pia iliweza kupita muda wa dakika tatu mpaka tano anajitokeza mpiga
kura mmojammoja kama anavyozungumza msimamizi Romanus Charles.
Wengi waliojitokeza katika uchaguzi huo
ni wazee wenye umri mkubwa na wakina mama wenye umri wakati, hata hivyo
wagombea pia walijitokeza kupiga kura na wakawa na ujumbe huu.
Jimbo la Lulindi linawapiga kura elfu 59
miasita 19 huku likiwa na vituo vya kupigia kura 199, kata kumi na nane,
limelazimika kurudia uchaguzi baada ya jina la mgombea ubunge wa CUF kukosewa.
Chanzo ITV