Wednesday, December 9, 2015

Mikoa 23 Kati ya 26 Yaanza Kuendesha Vikao Kwa Video



 Mikoa 23 kati ya 26 nchini, imekwishaanza kutumia mfumo kuendesha vikao na mikutano kwa njia ya video (video conference) ili kuipunguzia serikali gharama.
 
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (Utumishi), Hab Mkwizu, alisema hayo jijini Dar es Salaam jana na kusisitiza kwamba utaratibu huo  utaokoa fedha za posho walizotakiwa kulipwa washiriki, mafuta na muda.
 
Alisema vikao viwili viliwaunganisha kwa njia ya video halmashauri zaidi ya 26, huku wakuu wa idara, wakurugenzi, makatibu tawala, waliendesha vikao hivyo kwa mfumo huo.
 
Mkwizu alisema vikao na mikutano mingi inayofanywa katika eneo moja, gharama kubwa hutumika kuwasafirisha kwa njia ya magari na kuwalipa posho washiriki kuhudhuria mikutano hiyo.
 
“Matumizi ya kuendesha vikao kwa ‘video conference’ ni mzuri, hupunguza gharama kwa serikali, kunakuwa hakuna haja ya kuwasafirisha watendaji,” alisema.
 
Hata hivyo, alisema mikoa mipya mitatu ya Geita, Njombe na Simiyu, bado haijaanza kutumia mfumo huo kutokana na kutofungiwa kifaa maalum na hivi karibuni kitafungwa.

Chanzo: Nipashe