Friday, December 4, 2015

NEWS: Kiama Cha Magufuli Chahamia Kwenye mitandao Ya Kijamii

Mkurugenzi wa idara ya Habari
SERIKALI imeziomba nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), kuhakikisha zinakuwa na mfumo wa kuangalia matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ili isiendelee kusababisha madhara katika jamii.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene alisema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati akifunga mkutano wa 10 uliowashirikisha wadau wa utangazaji kwa njia ya digitali kutoka nchi za SADC. Alisema mitando ya kijamii kwa sasa inatumiwa vibaya na hivyo kuhatarisha amani na usalama wa nchi na wananchi wake.
Aidha, alisema mitandao hiyo ya kijamii, imekuwa ikisababisha kuporomoka kwa maadili na hivyo kuharibu watoto na jamii ambayo imekuwa ikitumia mitandao hiyo kwa njia zisizohalali na kujifunza mambo ambayo huchangia kuharibu tabia.
Aliziomba nchi hizo kuhakikisha zinatumia teknolojia hiyo, kuonesha vipindi vya Afrika vinavyoonesha taswira ya Afrika, badala ya kuonesha kwa wingi vipindi vya Magharibi. Mkutano huo ulifanyika kwa siku mbili Dar es Salaam na ulijadili mambo mbalimbali.
Chanzo HabariLeo