Friday, January 22, 2016

JOB VACANCY: Tangazo la Ajira Serikalini


CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA SERIKALI NA AFYA TANZANIA (TUGHE)
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Katikbu Mkuu wa TUGHE anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi

1. Katibu Wa Mkoa – NAFASI NNE (4)

MAJUKUMU YA KAZI

• Mshauri Mkoani kwa vikao vya Mkoa.
• Kupanga, kusimamia, kudhibiti na kuratibu shughuli za Chama Mkoani.
• Kusimamia Mipango ya utafiti na utayarishaji wa Makala kulingana na maagizo ya vikao vya chama mkoani/Taifani.
• Kusimamia Fedha na mali za chama mkoani.
• Kumwakilisha katibu mkuu katika vikao mbalimbali mkoani vitakavyohisika.
• Kiongozi wa watumishi wote wa TUGHE Mkoani.
• Katibu wa TUGHE wa Mkoa.
• Kujadiliana na kufunga mikataba ya Hali Bora za Kazi na Waajiri.
• Kufanya Kazi atakayopangiwa na katibu Mkuu.

SIFA ZA MWOMBAJI

• Kuajiriwa Mtu/Mwanachama mwenye Elimu ya Shahada ya Chuo Kikuu katika fani ya Sheria, Utawala, au Sheria za kazi.
Sifa za Ziada
• Awe mwenye kujituma katika kazi bila kusimamiwa.
• Awe mbunifu.
• Awe mwenye kutimiza majukumu yake kwa usahili na kwa wakati.
• Awe mwaminifu.
• Mwenye utayari wa kujifunza na kufundishka.
• Awe tayari kufanya kazi mkoa wowote wa Tanzania Bara.
• Mwanachama wa TUGHE atafikiriwa zaidi.

Uzoefu

• Mwenye uzoefu usiopungua miaka miwili katika shughuli za vyama vya wafanyakazi.

Mshahara
Kwa kuzingatia viwango vya Mishahara kulingana na Muundo wa Utumishi wa TUGHE.

NB: Masharti ya Jumla kwa Waombaji Wote

• Umri wa kila mvombaji awe na umri usiozidi miaka 45 ya kuzaliwa.
• Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani na namba za Simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
• Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya Taaluma, Vyeti vya Kidato cha nne na cha sita, vyeti vya kuzaliwa na vyeti vya kuzaliwa na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika pamoja na picha mbili (2) za passpoti.
• Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 05/02/2016.

APPLICATION INSTRUCTIONS:

Maombi yote yatumwe kupitia Posta kwa anuani ifuatayo:-

Katibu Mkuu
TUGHE Makao Makuu
S.L.P 4669
DAR ES SALAAM