Monday, March 21, 2016

Watatu wafariki kwenye nyumba ya kulala wageni (GUEST)

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida watatu ambao ni wafanyabiashara kutoka kata ya Manda wilayani Ludewa mkoa Njombe,wamekutwa wamekufa katika chumba kimoja huku miili yao ikiwa imechomwa moto kwenye nyumba ya kulala wageni  wilayani Kyela mkoani Mbeya na kuzua Taharuki kwa wakazi wa eneo hilo.
Tukio hilo ambalo ni la kikatili limetokea wilayani hapo majira ya saa kumi alfajiri baada ya mama mmoja ambaye ni jirani na nyumba hiyo alipoona moshi unafuka kwenye chumba hicho na kutoa taarifa kwa mmiliki wa nyumba hiyo ambaye alitoa taarifa polisi na kuvunja mlango wa chumba hicho.
Akizungumza na Chanzo chetu,mmiliki wa nyumba hiyo ya kulala wageni,Crisprian Mtengela amesema aliwapokea watu hao na kuwapangisha vyumba huku wakianza kunywa pombe wakiwa pamoja na kesho yake likapatikana tukio hilo ambalo ni la kwanza kutokea tangu aanze kazi hiyo.
Mganga mfawidhi wa wilaya hiyo, Fransis Muhagama ,licha ya kukiri hospitali yake kupokea miili ya watu hao amesema,hawezi kutoa majibu kwa sasa hadi uchunguzi kamili utakapokamilika na kwamba walikutwa na kamba shingoni.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya kamishna msaidizi Ahmad Msangi,akiongea na Chanzo chetu ofisini kwake amekiri kutokea kwa tukio hilo,huku akidai kwamba tayari wanamshikiria mmiliki wa nyumba hiyo ya kulala wageni kwa uchunguzi zaidi.
Chanzo: Chanelten