Saturday, April 2, 2016

Afikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa mwaka 1 na nusu, Mtwara.

Mtuhumiwa wa ubakaji aliyefahamika kwa jina la john  Nkondola mkazi wa manispaa ya Mtwara Mikindani  amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara  kwa kosa la kumbaka na kumlawiti mtoto wake wa kufikia  mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.

Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Emily Mwambapa, Mwendesha mashtaka wa serikali Peter Museti amesema  kulingana na vifungu vya kanuni ya adhabu kama ilivyofanyiwa marekebisho  na sheria ya mwaka 2002, mtuhumiwa John Nkondola  anatuhumiwa kwa kosa kumuingilia kimwili mtoto wa mwaka  mmoja na nusu wakati shtaka la pili mtuhumiwa anashtakiwa kwa kosa la kumlawiti mtoto huyo huyo kinyume na maumbile kulingana na vifungu vya kanuni ya adhabu vilivyofanyiwa marekebisho na sheria ya mwaka 2002.
 
Hata hivyo mtuhumiwa amekana mashtaka yote mawili na amerudishwa rumande baadaya kukosa wadhamini 2 wa kusaini hati ya dhamana ya shilingi milioni 4 kila mmoja, na kesi imetajwa kusikilizwa tarehe 11-04 -2016.
Kwa upande wake mama mzazi wa mtoto aliyefanyiwa kitendo hicho Salome Juma ameomba Jamhuri kufanya kazi yake, huku akisisitiza kitendo alichofanyiwa mtoto wake ni cha kinyama.