Monday, April 18, 2016

Binti Anajisiwa Kwa zamu Kisha auawa


WATU wawili wamekufa katika matukio mawili katika Mkoa wa Katavi, likiwemo la mtoto wa kike wa umri wa miaka tisa aliyeuawa kwa kucharangwa mapanga na watu wasiofahamika baada ya kumnajisi kwa zamu.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Paza Mwamlima ameliagiza Jeshi la Polisi wilayani humu kuhakikisha linawasaka na kuwatia mbaroni watu wasiofahamika ambao wanadaiwa kumnajisi na kumuua mtoto huyo.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa mkasa huo ulitokea Aprili 14, saa 6:00 mchana katika kijiji cha Kapanga wilayani humu baada ya mtoto huyo kuagizwa na babu yake, Maela Mayanga (58) kwenda shambani ili akafukuze tumbili waliovamia kijiji hicho wanaokula mahindi yaliyopo shambani.

Inadaiwa kuwa mtoto huyo baada ya kulinda tumbili wasile mazao shambani kwa muda mrefu ndipo babu yake alipomwagiza kaka wa mtoto huyo aende shambani ili mtoto huyo arudi nyumbani kwa ajili ya chakula.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa shamba la mzee Mayanga halikuwa mbali na kijiji hicho. Inaelezwa kuwa kaka huyo alipofika shambani hakumwona dada yake, hata alipomwita kwa kupaza sauti hakuitikiwa, ndipo akaanza kumtafuta akiamini alikuwa amejificha na anacheza mchezo wa kujificha.

“Lakini baada ya kutafuta kwa muda mrefu alikata tamaa na kurejea kutoa taarifa nyumbani kuwa hakumwona dada yake huyo,” alieleza mtoa taarifa.

Baadhi ya mashuhuda kwa masharti ya kutoandikwa majina yao gazetini walieleza kuwa baada ya mzee Mayanga kupata taarifa hiyo aliambatana na mjukuu wake huyo wa kiume, walienda shambani ambapo walimtafuta kwa muda mrefu bila mafanikio hivyo wakakata tamaa wakirejea kijijini.

Kwa mujibu wa Mzee Mayanga, aliamua kwenda na mwalimu wa dini wa Kanisa Katoliki kijijini humo ambaye aligonga kengele ambapo waumini wa kanisa hilo wakakusanyika kwa wingi.

Mzee Mayanga aliwasimulia kisa chote ndipo kundi kubwa la waumini hao walielekea shambani na kuanza kumsaka mtoto huyo kwa zaidi ya saa tatu ndipo waliupata mwili wa mtoto huyo ukiwa umetupwa kando ya mto karibu na mashamba ya kijiji hicho.

Baada ya kuukagua mwili huo ilibainika kuwa mtoto huyo alinajisiwa kwani alikuwa amechanika vibaya sehemu za siri akiwa na majeraha makubwa kifuani. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Rashid Mohamed alikiri kutokea kwa tukio hilo, akiapa kuwa Polisi itafanya kila liwezekanalo ili watuhumiwa wakamatwe na hatua za kisheria zichukue mkondo wake.

Katika tukio lingine lililotokea Aprili 13, mwaka huu saa 5:00 usiku, Shukuru Korongo (32) ameuawa kwa kupigwa na rafiki yake Pisikitu Maiko (30), wakigombea viroba vya pombe kali iitwayo Zed katika sherehe iliyofanyika kwa jirani yao katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda alieleza kuwa wakati marafiki hao walipokuwa wakinywa pombe hiyo kali, Maiko aliwahi kumaliza na alimuomba Shukuru amgawie viroba vya pombe hiyo kali