Saturday, April 9, 2016

Mtu Mmoja Avamiwa na Kukatwa Miguu



Katika hali ya kusikitisha mtu mmoja aitwaye Juma Bakari mkazi wa kijiji cha Mkamba wilaya ya Kilombero amenusurika kifo na kujikuta akiwa hana miguu yote miwili mara baada ya kuvamiwa na watu wasio julikana ambapo walimshika na kumkata miguu kisha kuondoka nayo huku wakimtelekeza katika mashamba ya kiwanda cha miwa(ILOVO).

Akizungumza na ITV kwa masikitiko makubwa wakatia akiwa amelazwa katika Hospitali ya Mtakatifu Francisco iliyopo mji mdogo wa Ifakara, majeruhi wa tukio hilo Juma Bakari ameeleza namna ambavyo alikumbwa na kadhia hiyo wakatia akitoka kumsindikiza rafiki yake aliyejulikana kwa jina moja la Hamza na kushambuliwa na watu hao.
 
Nao ndugu wa majeruhi huyo akiwemo mkewe Basilisa Sprian wameeleza kusikitishwa na kitendo kibaya alichofanyiwa ndugu yao huku wakiomba msaada wa hali na mali utakaosaidia kuyanusuru maisha ya kijana huyo.
 
Kwa upande wake mganga wa zamu wa hospitali hiyo amekiri kumpokea majeruhi huyo akiwa katika hali mbaya huku Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro Ulirich Matei amethibitisha kutokea kwatukio hilo ambapo amesema Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kubaini  chanzo cha tukio hilo.