Friday, April 1, 2016

Watu Watatu wapoteza maisha Mkoani Tabora.


Watu watatu wamepoteza maisha kwa nyakati tofauti, katika wilaya za Urambo Kaliua na Igunga Mkoani Tabora huku mmoja akikatwakatwa kwa kitu chenye ncha kali, huku mwanamke  akiuawa kwa fimbo na mmewe, na na mtoto wa miaka tisa akifa kwa kupigwa radi akiwa anachunga mifugo.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkoani Tabora Kamanda wa Polisi Mkoani humo Kamishina Msaidizi Hamisi Suleimani, amekemea tabia ya wafugaji ambao hawawapeleki watoto shule na kuwapeleka kuchunga mifugo, jambo ambalo limesababisha kifo cha mtoto huyo. 
 

Aidha katika hatua nyingine Kamanda Hamis Suleimani amewataka wananchi Mkoani Tabora kuanzia tarehe 01/04/ mwaka huu 2016 wote wanaomiliki silaha kama ni halali kuzisajili upya, na kama sihalali basi watumie fursa hii kuzisalimisha maeneo yanayotambulika, na hapatakuwepo na masharti ya aina