Sanjari na uchaguzi huo, JKT
limewapangia makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo kwa muda wa miezi
mitatu na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 01 – 05 Juni
2016.
Vijana waliochaguliwa, wamepangiwa
katika Kambi za JKT Rwamkoma – Mara, JKT Msange – Tabora, JKT Ruvu –
Pwani, JKT Makutupora – Dodoma, JKT Mafinga – Iringa, JKT Mlale –
Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba – Tanga, JKT Bulombora, JKT Kanembwa
na JKT Mtabila – Kigoma.
Aidha, wahitimu wenye ulemavu wa
kuonekana kwa macho (physical disabilities) wanatakiwa kuripoti Kambi ya
JKT RUVU, iliyopo Mlandizi mkoani Pwani, ambayo ina miundombinu ya
kuhudumia watu wa jamii hiyo.
JKT linawataka vijana hao kuripoti
makambini wakiwa na nguo za michezo kama vile ‘track suit’, bukta, raba
pamoja na nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa kwenye makambi yenye
baridi kama JKT Makutupora, JKT Mafinga, JKT Mlale, JKT Kanembwa na JKT
Mtabila.
Mkuu wa JKT anawakaribisha vijana wote
waliochanguliwa ili waweze kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza
uzalendo, umoja wa kitaifa, uhodari, stadi za kazi, stadi za maisha na
utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa letu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya JKT
Tarehe 20 Mei 2016