Wednesday, June 22, 2016

Atupwa Jela maisha Kwa Kubaka katoto ka darasa la Pili

 
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala, imemhukumu kifungo cha maisha jela, Siasa Mwinyi (40) baada ya kupatikana na hatia ya kumnajisi mtoto wa miaka tisa ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili. Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassan alisema Mahakama imeridhishwa na yaliyoelezwa na mashahidi wanne.
Mshtakiwa alitenda kosa hilo Januari mwaka huu katika eneo la Tabata Kisukuru katika Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam. “Makosa ya ukatili yamekuwa ni mengi na hatujui tatizo ni nini kwa sababu kila kukicha watoto wanafanyiwa ukatili na unyama wa namna hii na mambo kama haya yanapaswa kulaaniwa na kila mtu,” alisema hakimu huyo.
Kwa mujibu wa hakimu, ushahidi uliotolewa na mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi Magoza iliyopo Tabata Segerea, Mwinyi alikuwa akimwingilia kila mara wakati alipokwenda nyumbani kwa mshitakiwa huyo kunywa maji.
Alidai mshitakiwa alikuwa akimnajisi mtoto huyo mara kwa mara katika migomba wakati akitoka shuleni na watoto wenzake. Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Wakili wa Serikali, Agatha Lumato aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali dhidi ya mshitakiwa huyo kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo.
Hata hivyo, Mahakama ilitoa nafasi kwa mshitakiwa aeleze kwa nini asihukumiwe ambapo alijitetea kwa kuiomba Mahakama impunguzie adhabu kwa sababu ana mke na watoto watano wanaomtegemea na pia hajui kusoma wala kuandika.

MATUKIO ZAIDI YA KUSISIMUA BOFYA HAPA>>