Thursday, July 7, 2016

Atupwa Kortini kwa Kumuua mtoto wake

 
Mkazi wa Kijiji cha Mumiramira, Kata ya Bugara Paschal Kabiti (34), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ngara, kwa tuhuma za kumchapa fimbo mtoto wake mwenye umri wa miezi minne na kusababishia kifo.
Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Jumanne Maatu amedai juzi kuwa mshtakiwa alitenda kosa Juni 26, alipokuwa kigombana na mkewe Livia Kabuti aliyekuwa amembeba mtoto mgongoni.
Mstakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji, hivyo Hakimu Andrew Kabuka aliahirisha kesi hadi Julai 12.