Friday, July 15, 2016

Kijana auwawa na walinzi wa mwekezaji Msitu wa Mbogo wilayani Arumeru.

Taharuki kubwa imewapata wananchi wa kijiji cha Msitu wa Mbogo wilayani Arumeru baada ya tukio la kupigwa risasi kijana mmoja mkazi wa kijiji hicho na askari wanaodaiwa kuwa walinzi wa shamba la mwekezaji na kupoteza maisha baada ya jitihada za kuokoa maisha yake kushindikana.

Wakizungumza wakati wa ibada ya mazishi ya kijana huyo Peter Kimaro ambaye pia dada yake Bi Lilian Kimario aliyekuwa na ujauzito wa miezi nane alipoteza maisha kwa mshtuko wa taarifa za msiba wa kaka yake wananchi hao wameiomba serikali kumaliza mgogoro na mwekezaji wa shamba la Tanzania Plantation mgogoro ambao wanaeleza kuwa mpaka sasa umeshasababisha vifo vya watu watatu.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Bwana Willy Njau anasema tangu mgogoro huo umeanza kufukuta  miaka ya themanini bado hakuna suluhisho la kudumu hali anayoieleza kuwa inachangiwa na kutokutekelezwa kwa azma ya serikali ya kuyafutia hati za umiliki mashamba yasiyoendelezwa.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya Alexanda Mnyeti amehudhuria mazishi hayo ambapo analiagiza jeshi la polisi kuwakamata haraka wale wote waliohusika na tukio hilo.

MATUKI ZAIDI YA KUSISIUA BOFYA HAPA>>