Friday, July 1, 2016

Watu 11 wamefariki wengine kujeruhiwa katika ajali Morogoro,



Watu 11 wamefariki dunia Na wengine ambao idadi yao haijajulikana Mara moja wamejeruhiwa baada ya kutokea kwa ajali Mbili tofauti katika eneo la njia panda ya Veta Wami Dakawa,tarafa ya Magole wilayani Kilosa, katika barabara kuu ya Morogoro-Dodoma zikihusisha Magari makubwa matatu kugongana uso kwa uso,kuwaka moto na kupinduka.

Taarifa zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Ulrich Matei aliyefika eneo ka tukio zimesema ajali yà kwanza ilihusisha gari ndogo aina ya Noah ambayo haijakutwa eneo la tukio ambayo ilikuwa ikijaribu kulipita Lori lililokuwa limebeba kontena lenye mchele Na vitunguu likitokea uelekeo wa Dodoma kuelekea Morogoro.

Akabainisha kuwa Noah mbele ikakutana Na Lori la mafuta (tanker) ambalo katika kujaribu kuikwepa Noah ikakutana uso kwa uso na Lori lililokuwa likikokota kontena lenye mchele Na Magari hayo kuwaka moto Na kupinduka.

Amesema katika ajali hiyo,wàtu watano wamepoteza maisha wakiwemo wanawake wawili waliokuwa abiria ndani Ya Lori lenye kontena, Na Mtu mwingine mmoja pamoja Na maiti nyingine tatu ambazo hazikutambuliwa ni za kina Nani baada ya kuungua vibaya.

Kamanda Matei amesema wakati jitihada za Askari polisi kwa kushirikiana na kikosi cha zimamoto wakiendelea na shughuli za uokoaji eneo la ajali hiyo iliyotokea kuanzia Juni 30,majira ya saa 11 jioni, ilipofika Julài Mosi majira ya saa 10 alfajiri ilitokea ajali Nyingine iliyohusisha basi la abiria.

Amesema ajali hiyo ilihusisha basi la abiria Mali ya kampuni ya Ota High Class yenye namba za usaliji T 201 DGK iliyokuwa ikitokea Bukoba kuelekea Jijini Dar es salaam ambayo kutokana Na mwendo kasi dereva wake alishindwa kumudu Na kuligonga Lori la mafuta lililopata ajali YA awali Na kupinduka.

Katika ajali hiyo iliyohusisha basi,wàtu sita wamepoteza maisha papo Hapo Na wengine ambao idadii yao hakijaweza kujulikana Mara moja walijeruhuwa nna kukimbizwa hospitali ya Rufaa YA Mkoa wa Morogoro Na kituo cha Afya Dumla kwa matibabu.

Mmoja wa mashuhuda waliokutwa eneo la Tukio,Japhet Suleiman,mkàzi wa Dakawa ambaye ni mwendesha pikipiki za abiria katika eneo hilo,anasema alikuwa Na wenzake,wakiwa watatu,walitoka kuwapokea abiria waliokuwa kwenye Noah na wakastukia mahindi Mkubwa ulioambatana Na moto,ambapo mwenzao mmoja anayejulikana maarufu kwa jina la Simba alishindwa kujiokoa na kupoteza maisha hukummwingine akijeruhiwa usoni.
Aidha Sultan Hamis Suleiman amesema alipata taarifa za ajali ya gari ya Mjomba wake,ambayo ndio ilitokea Na mchele ikitokea Mtukula kuelekea jijini Dar,ambapo alikiri vifo vya abiria wanawake wawili na mtu mwingine mmoja ambayo hajamtambua bado,Katika gari hiyo,huku  msmamizi wa gari hiyo  Said Saum Said  akinusurika na amepelekwa Jijini Dar es salaam kwa matibabu baada ya kujeruhiwa vibaya.

Mwandishi wa Habari hizi ameshuhudia Magari yaliyohusika nà ajali katika eneo la tukio,ambapo lori lililokuwa na mchele likiendelea kufuka Moshi kutokana ña Bidhaa zilizokuwemo kuungua Sambamba na Lori, basi la Ota lililokuwa limesogezwa pembeni ya barabara kupisha Magari kupita barabara kuu ya Morogoro Dodoma kukiwa limefutwa kabisa palipokwa na jina kwa kutumià kemikali,mabaki ya kichwa cha tanker na pikipiki tatu zilizoungua kabisa.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk Kebwe Stephen Kebwe ambaye naye amefika eneo la tukio,amelaani vikali kitendo Madereva wanaoendesha bila kufuata Sheria,kanuni Na taratibu za usalama barabarani,na kuwataka wananchi kukaa Mbali Na eneo la ajalli Na wasijaribu kuchota mafuta kwani eneo hilo sio salama,Sambamba na polisi kulinda usalama wa wananchi Na mali zao Na kuweka vizuizi kuepusha athari zaidi kujitokeza.

Kebwe pia amewaagiza wakala wa barabara Tanroads Mkoa wa Morogoro kumwaga mchanga katika eneo la ajali kudhibiti utelezi wa mafuta yaliyomwagika kwenye lami ili utelezi uliopo usisababishe ajali Nyingine zaidi.