Friday, December 30, 2016

Basi La National Express Lapata ajali na kupinduka mara 3 Singida

Watu wawili wamekufa na wengine ishirini na sita wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Singida, kufutia basi walilokuwa wakisafiria kupinduka mara tatu wilayani Mkalama.
Akithibitisha kutokea kwa vifo hivyo mganga mkuu wa hospitali ya mkoa wa Singida Daktari John Mwombeki amesema wamepokea majeruhi ishirini na sita maiti mbili moja ni ya dereva wa basi hilo Bwana Athumani Saidi na nyingine ni ya mama moja aliyetambulika kwa jina moja Janeth ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi Maluga wilayani Iramba na majerhi wanaendelea kupatiwa matibabu huku wengine wakipelekwa hospitali ya rufaa ya Muhimbili.
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida kamishina msaidizi wa polisi ACP Debora Daud Magiligimba amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa moja kasorobo na kuhusisha basi namba T 662 DEF Yunton kampuni ya National Express lilokuwa likitokea Iramba na kuelekea Dar-es-Salaam na chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva na kuto kuzingatia sheria za barabarani, huku akitoa wito kwa madereva hasa nyakati hizi za mwisho wa mwaka.    

MATUKIO ZAIDI YA KUSISIMUA BOFYA HAPA>>