Thursday, March 23, 2017

Hii ndiyo kauli ya Wema Sepetu Baada ya Nape Nnauye kutenguliwa Uwaziri


MSANII wa filamu nchini Wema Sepetu, ‘Madam’, ambaye hivi karibuni alihamia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ameweka ujumbe kwenye mitandao ya kijamii akionesha kuzipokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za mabadiliko madogo katika baraza la mawaziri yaliyofanywa na Rais Magufuli.

Wema ameweka ujumbe huo sambamba na picha tofauti tofauti za aliyekuwa Waziri wa Habari na Utamaduni, Nape Nnauye baada ya kutenguliwa na nafasi yake kuchukuliwa na Dk. Harison Mwakyembe.