Tuesday, March 7, 2017

Mwanamke Aishi na Mwanaume aliyekufa kwa miaka sita

Mwanamke mmoja amechanganyikiwa baada ya kugundua kuwa amekuwa akiishi na 'mume aliyekufa' kwa miaka sita!
Mwanamke huyo anayetambulika kama Grace Amadi alisema kuwa amekuwa akiishi na wanawe wawili, pamoja na mwanamume ambaye amepewa ushahidi kuwa alifariki mwaka wa elfu mbili na mbili.
Kulingana na mama huyo, amekuwa akiishi na mumewe 'Tony' kwa miaka sita na kupata watoto wawili, mmoja mwaka elfu mbili kumi na moja na mwingine mwaka elfu mbili kumi na tatu, na kuongeza kuwa 'Tony' amekuwa mume wa kawaida tu, anayetoka kuenda kazini kila asubuhi.
Grace alijua kuhusu 'kifo' cha mumewe alipopata mgeni aliyedai kuwa dadake asubuhi moja baada ya mumewe kuenda kazini. Mwanamke huyo alimletea picha za zamani za mumewe, picha za harusi na hata za mwili wake alipofariki mwaka elfu mbili na mbili pamoja na picha za mazishi ya 'Tony.'
Grace alishangaa kuona kuwa kweli, picha hizo zilikuwa za mumewe na kila kitu alichoambiwa na mwanamke huyoi kumhusu mumewe kilifanana na yale aliyoyajua kumhusu, kulingana na Naij.com

Mwanamke huyo pia alimletea picha za ajali iliyosemekana kusababisha kifo cha Tony mwaka elfu mbili na mbili.
Baada ya majirani kutia shaka habari hizo, walijaribu kupiga simu kazini kwa jamaa huyo na kushangaa walipoambiwa kuwa hakuwa mfanyakazi wa kampuni hiyo.
Kulingana na Naij.com, Grace alipelekwa kwa mganga ambako anatarajiwa kufanyiwa taratibu za kitamaduni.