Akikabidhi taarifa hiyo kwa Rais Magufuli, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Utumishi na Utawala Bora, Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki, Rais amesema kuwa, Wizara yake iliagiza NECTA kuhakiki vyeti vya kidato cha nne, cha sita na vya uwalimu.
“Jumla ya watumishi wa umma 435,000 wamefanyiwa uhakiki wa vyeti vyao vya taaluma, Watumishi 9932 kati ya watumishi waliohakikiwa walikutwa na vyeti vya kughushi, Vyeti vyenye utata. Vyeti 1538 vilikuwa vikitumiwa na jumla ya watu 3076”
Akihutubia
baada ya kupokea taarifa hiyo, Rais Magufuli amewataka watumishi 9,932
waliobanika kuwa na vyeti vya kugushi waondoke kazini mara moja, na
kuagiza mamlaka zilizowaajiri kukata mishahara yao huku akiongeza kuwa
kwa wale watakaobakia kazini hadi Mei 15, wakamatwe ili sheria ichukue
mkondo wake ikiwemo kufungwa jela miaka 7.
“Mtu aliyeghushi vyeti hatuwezi kumsamehe, wote ataondoka mara moja, mishahara yao ikatwe kabisa”
“Hao
watumishi 9,932 wenye vyeti feki wenyewe kazini mara moja, watumishi
wenye vyeti feki ambao watakaidi na kubaki kwenye ajira hadi Mei 15,
wakamatwe wafikishwe kwenye vyombo vya sheria wafungwe hiyo miaka 7.
“Wanaotumia
cheti kimoja watu wawili, wasiwekewe mshahara ya mwezi huu, na kama
wanajijua wajisalimishe, pia nikuombe Waziri utangaze mara moja nafasi
za kazi 9,932 za watumishi wenye vyeti feki ambao wametakiwa kuondoka
mara moja kazini ili zichukuliwe na watu wengine wenye vigezo.” Alisema Rais Magufuli