Friday, April 28, 2017

Waziri Kairuki: Hawa Ndiyo Watumishi Waliohakikiwa Vyeti Vyao

DODOMA: Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Utumishi na Utawala Bora, Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki leo Aprili 28, 2017 amekabidhi kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli Taarifa ya Uhakiki wa Vyeti vya Watumishi wa Umma.


Akikabidhi taarifa hiyo kwa Rais Magufuli, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Utumishi na Utawala Bora, Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki, Rais amesema kuwa, Wizara yake iliagiza NECTA kuhakiki vyeti vya kidato cha nne, cha sita na vya uwalimu.


“Jumla ya watumishi wa umma 435,000 wamefanyiwa uhakiki wa vyeti vyao vya taaluma, Watumishi 9932 kati ya watumishi waliohakikiwa walikutwa na vyeti vya kughushi, Vyeti vyenye utata. Vyeti 1538 vilikuwa vikitumiwa na jumla ya watu 3076”

“Wizara yangu iliagiza NECTA kuhakiki vyeti vya kidato cha nne, cha sita na vya uwalimu.”
“Uhakiki huu haujafanyika kwa viongozi wa kisiasa kwa sababu wao wanahitajika kujua kusoma na kuandika tu.

“Pia Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Wabunge na Madiwani hawajahakikiwa vyeti vyao vya taaluma kwa kuwa mamlaka ya uteuzi ndiyo wanajua ufanisi wa kazi zao.

“Uhakiki wa vyeti umehusisha Makatibu Wakuu, Watendaji na maofisa wengine ndani ya serikali.

“Watumishi wenye vyeti halali ni asilimia 94 ya watumishi waliohakikiwa, baadhi ya watumishi waliwasilisha vyeti pungufu. Tumewaagiza walete vilivyosalia”


TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI BOFYA HAPA
http://studentswagas.blogspot.com/