Tuesday, May 23, 2017

Juve yamsajili Cuadrado kwa mkataba wa miaka mitatu

                              Juan Cuadrado                            
Timu ya Juventus ya Italia imemsajili winga Juan Cuadrado kwa mkataba wa miaka mitatu, wenye thamani ya pauni milioni 17.

Cuadrado amesajili na Juventus baada ya kucheza hapo kwa msimu miwili kwa mkopo akitokea klabu ya Chelsea ya nchini England.
Winga huyu ameichezea timu hiyo jumla ya michezo 83, baada ya kushindwa kufanya vizuri na Chelsea ambapo walimsajili kwa kiasi cha pauni million 23.3 akitokea Fiorentina.
Chini ya kocha Massimiliano Allegri Cuadrado ametwaa ubingwa wa Seria A mara mbili, kombe la Copa Italia mara mbili, na kuisaidi timu yake kufika fainali ya kombe la klabu bingwa ulaya mchezo utakaochezwa June 3
Habari zaidi za Kimichezo Bofya hapa

     TANGAZO 
http://studentswagas.blogspot.com