Thursday, May 11, 2017

Mwanafunzi Akamatwa na Bastola, Risasi 13

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph, Lazaro Mbise (23) anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kukutwa na bastola pamoja na risasi 13 ambayo alimwibia baba yake.

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema mwanafunzi huyo alipokamatwa alikiri kuiba bastola hiyo pamoja na fedha kiasi cha Sh800, 000.

“Bastola hiyo ni LUGER cz100 mtuhumiwa alikiri aliiba pamoja na risasi kutoka kwa baba yake,” amesema Sirro.


Kamishna Sirro ameagiza mzazi wa mtuhumiwa kukamatwa ili afikishwe mahakamani kwa kosa la kutohifadhi bastola yake vizuri.

Matukio zaidi ya Kusisimua BOFYA HAPA