Saturday, May 20, 2017

Mwili wa mwanasiasa 'wapatikana mtoni'

Polisi nchini Kenya wanasema mwanasiasa aliyehusishwa na uvamizi wa mashamba ya kibinafsi amepatikana ameuawa.
Wanaamini mwili uliotolewa mtoni hii leo ni wa Thomas Minito, ambaye alikuwa akichunguzwa kwa kujihusisha na kupigwa risasi kwa mhifadhi Mwitaliano Kuki Gallman.
Mwili huo ulipatikana ukielea kwenye mto mmoja eneo ya Machakos, kilomita hamsini mashariki mwa Nairobi.
Polisi wanasema walimtambua kupitia stakabadhi zilizokuwa mfukoni mwake. Familia yake hata hivyo haijadhibitisha haya.
Polisi wanasema wanashuku aliuawa kwa kuwa alikuwa na majeraha kichwani.
Minito alikamatwa tarehe 30 mwezi Machi na kushtakiwa kwa kosa la kuchochea ghasia katika kaunti ya Laikipia, yaliyofanya mhifadhi mashuhuru wa mazingira na mwandishi, Kuki Gallmann kupigwa risasi.
Polisi wangali wanafanya operesheni katika Kaunti ya Laikipia iliyoko Kenya ya Kati. Hii ni baada ya wafugaji kuvamia mashamba ya kibinafsi wakitafuta lishe. Mmiliki mmoja wa mashamba hayo makubwa aliuawa mapema mwezi Machi, Wafugaji wanadai polisi wamewauwa mamia ya wanyama ili kuwafurusha.
Chanzo: BBC

 MATUKIO ZAIDI YA KUSISIMUA BOFYA HAPA 


http://studentswagas.blogspot.com/