Katia mishe mishe za sherehe za mkesha wa sikukuu zilizokuwa
zikiendelea usiku wa kuamkia jumapili ya pasaka, Kamera ya mpigapicha
wetu wa Utamu Wa Raha ilinusurika kutolewa roho na wanadada ambao majina
yao hayakuweza kupatikana.
Mnamo
mida ya saa nane na robo usiku katika pitapita ya mpiga picha wetu huyo
katika maeneo ya Sinza jijini Dar aliingia kwenye CLUB moja ambapo
alielekea sehemu iliyokuwa na vibanda vya wateja ambavyo vimejificha.
Huko ndiko mpigapicha wetu alikumbana na tukio lililomshangaza na
kumuacha hoi. Kwakuwa alikuwa kazini hakutaka kupoteza muda. Aliseti
kamera yake na kusogea karibu na kibanda kile.
Kwa
bahati mbaya wakati anajiweka sawa alikanyaga kopo la maji safi ambalo
lilitoa sauti na kuwagutusha wadada hao. Kitu kilichofuata ni wadada hao
kuokota mawe na kuanza kumrushia mpiga picha wetu huku wakimporomoshea
matusi ya nguoni.
Hata hivyo mpiga picha wetu alifanikiwa kupata picha moja kama ambavyo inaonekana hapo juu.
