Monday, April 21, 2014

KASHFA YA USAGAJI YAMVAA MSANII WA BONGO MOVIE MAARUFU KAMA KAJALA MASANJA. ANASEMA KILA MWANADAMU ANAHAKI YA KUFANYA ANACHOKITAKA YEYE, KWAHIYO KAMA MNAONA ANACHOKIFANYA YEYE ANAKOSEA BASI ANAOMBA MUMTUKANE USIKU NA MCHANA.

 
 Msanii wa filamu Tanzania maarufu kama kajala amejikuta akiingia katika wakati mgumu baada ya mashabiki wake kumtupia lawama kuwa anajihusisha na tabia za msagaji. Kashfa hiyo ilianza pale msanii huyo
alipotupia picha akiwa na mtoto wake ndani ya gari. Kajala alipost picha hiyo kwenye mtandao wa Instagram huku akiisindikiza na maneno haya "With my twin tukifanya yetu". 

Kauli ya msanii huyo ilionekana kueleweka vibaya kwenye vichwa vya baadhi ya mashabiki wake ambapo walimjibu hivi  "mnafanya yenu yapi mnasagana tu". Maneno hayo makali yaliyotolewa na mmoja wa friends wake yalionekana kumkera sana Kajala pamoja na baadhi ya mashabiki wengine. Kitu ambacho kilifuata hapo kilikuwa ni maneno machafu dhidi ya wanaomtuhumu kajala kuwa msagaji na wanaomtetea.

Kajala mwenyewe alionekana kuchanganywa sana na kashfa hiyo jambo ambalo lilimfanya kuandika post nyingine ambayo inasomeka hivi "nadhani kila binadamu anafanya kitu anachokipenda, lakini kama ninyi nyote mnaona ninachokifanya nakosea, siwezi kuwalaumu naomba mnitukane usiku kucha mkilala mnitukane, mkiamka nitukaneni nimeshazoea. nilikuwa naumia mwanzo lakini sasa siumii tena. ninachowaomba hamjui nimepata tabu gani na mwanangu kwaiyo kama anayewakosea ni mimi nasio mtoto wangu basi naomba mnitukane mimi na umaya wangu msimuingize mwanangu please nawaomba sana kiroho safi.

HAPACHINI NI PICHA ZA KAJALA AKIWA PAMOJA NA MTOTO WAKE