Monday, May 19, 2014

WANANCHI WENGI WAMEPOTEZA AJIRA KUTOKANA NA MILIPUKO YA MABOMU

 
Kufuatia mfurulizo wa milipuko iliyotokea hivi karibuni nchini Kenya hasa katika maeneo Nairobi na Mombasa ambapo watu kadhaa walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa.


Afisa mkuu wa kampuni ya shirika la kampuni inayoshughulikia masuala ya utalii nchini humo, Kenya Tourism Federation, Agatha Juma, amesema kuwa kupungua kwa utalii nchini kutasababisha wananchi wengi kupoteza ajira, hasa kwa wale ambao wanafanya kazi katika hoteli mbalimbali za kitalii.


Usalama umeimarishwa katika maeneo mbalimbali kama vile kwenye ubalozi wa Marekani na kwenye ofisi za Umoja wa mataifa Nairobi. Pia kumechukuliwa hatua madhubuti kuhakikisha misongamano ya watu inapungua katika maeneo hayo.