Friday, February 27, 2015

Askari Ajeruhiwa Kwa kupigwa na Mapanga na Nondo



Baada ya vuta nikuvute kati ya Askari na wana ndugu hao ndipo wana ndugu walipoamua kumshambulia askari huyo kwa kumpiga na panga Kivuyo kwenye miguu na mikono kisha kumpiga kwa nondo kichwani.

Mtu mmoja mkoani Tanga wilayani Kilindi katika kijiji cha Kwamazandu, aliefahamika kwa jina la Godfrey Kivuyo (34) askari wa jeshi la Mgambo, amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa na mapanga kwenye miguu, mikono na kupigwa nondo kichwani.

Bwana Kivuyo amekumbana na kipigo hicho alipokuwa amekwenda kumkamata Mtuhumiwa Omari Bakari (34) ambaye alikuwa akikabiliwa na kesi ya mgogoro wa ardhi. Kwa mujibu wa chanzo chetu kimeeleza kuwa Bwana Kivuyo alipofika nyumbani kwa mtuhumiwa huyo alikutana na ndugu zake ambao waligoma kukamatwa kwa ndugu yao Omary.

Baada ya vuta nikuvute kati ya Askari na wana ndugu hao ndipo wana ndugu walipoamua kumshambulia askari huyo kwa kumpiga na panga Kivuyo kwenye miguu na mikono kisha kumpiga kwa nondo kichwani.

Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo Juzi saa 10:30 Jioni katika kijiji cha Kwamazandu. Amesema kuwa, Watuhumiwa wote sita wanashikiriwa na jeshi la polisi kwaajili ya kujibu shitaka hilo.  

Watu ambao wanashikiliwa kuhusiana na tukio hilo ni pamoja na Omari Bakari (38), Abdala Bakari (35), Haji Mohamedi (21), Halima juma (28), Mwajabu Salim (35), na Mohamed Seleman (34), wote hao ni wenyeji wa Kwamazandu wilayani Kilindi.