Saturday, February 28, 2015

Hiki ndicho kilichomuua Kapteni John Komba


  
             Kapteni John Komba enzi za Uhai wake
Habari zilizotufikia hivi punde ni kuwa Kapteni John Komba amefariki dunia katika Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam.

Mtoto wa marehemu Mr. Jerry Komba amezungumza na chanzo chetu na kusema kuwa kifo cha baba yake kimetokana na tatizo la sukari. Ameeleza kuwa sukari ilishuka ghafla alipokuwa nyumbani kwake Mbezi Beach jijini Dar es salaam.


“Ni kweli mzee amefariki dakika 50 zilizopita. Alikuwa ameketi nyumbani na ndipo ghafla sukari ilishuka na baada ya muda mfupi alifariki dunia” alisema Jerry Komba mtoto wa marehemu.



Mpaka kufa kwake Kapteni John Komba alikuwa Mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmasauri Kuu ya CCM Taifa na Kiongozi wa bendi ya TOT.

"Bwana alitoa, Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe"