Monday, March 16, 2015

CHANZO CHA KUTEKETEZWA NA MOTO BWENI LA MABIBO HOSTELI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM CHABAINIKA

 
 Mwanafunzi wa kike Aruka kutoka ghorofa ya pili ili kuokoa maisha yake baada ya kuona moto huo. Mwanafunzi huyo apata majeruhi na kukimbizwa kwenye dispensari ya Hosteli hapo kwa matibabu.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo ni kwamba chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme ambayo imeanzia kwenye chumba cha kuhifazia magodoro.

Wanafunzi wa chuo hicho ambo ni wakazi katika mabweni hayo ya Mabibo wameeleza kuwa siku za karibuni kumekuwa kukitokea shoti katika chumba hicho.

Vilevile chanzo cha habari hii kimeeleza kuwa hakuna mtu ambaye amepoteza maisha kutokana na ajali hiyo.  

Lakini mwanafunzi mmoja aliyefahamika kwa jina la Cesilia ni majeruhi ambaye aliumia baada ya kuruka kutoka ghorofani ili kuokoa maisha yake. Mwanafunzi huyo amefikishwa kwenye dispensari ya hosteli hapo kwaajili ya matibabu.

Mhadhiri wa Chuo cha Dar es alaama amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa wanafunzi wote waliokuwa wakiishi katika bweni hilo watapatiwa sehemu ya kulala hadi pale usalama utakapohakikishwa katika ghorofa ya kwanza na ya pili ambazo hazikuathirika na ajali hiyo.