Saturday, March 21, 2015

Mwanamke Ajinyonga baada ya kukutwa na Mtoto wake wa miaka 5 Akifanya mapenzi

Mwanamke mmoja aliyafahamika kwa jina la Ester nchini Nigeria hivi karibuni amechukua uamuzi wa kujitoa uhai wake baada ya kubainika kusaliti ndoa yake.

Kwa habari zilizotoka kwa mwanaume wa mwanamke huyo alieleza kuwa, mke wake alikuwa ni mrembo sana kiasi cha kuwavutia wanaume wengi kumhitaji kimapenzi. Kitendo hicho kilipelekea hata mke wake kumuonesha baadhi ya wanaume ambao walikuwa wakimtaka.

Pamoja na changamoto zote hizo lakini mwanaume huyo aliendelea kumuamini mke wake kwa kumuona kuwa alikuwa ni muaminifu na mwenye kuchunga ndoa yake.

Uzuri aliokuwa nao mwanamke huyo ulimpa changamoto nakujikuta akichepuka pamoja na kwamba alikuwa akiaminiwa sana na mume wake. 

Siri hyo ilifichuliwa na mtoto wao wa miaka mitano ambaye alishuhudia mama yake akichepuka na mwanaume mwengine mbali na baba yake. Baada ya mtoto huyo kushuhudia mchezo mchafu wa mama yake alikwenda kumueleza baba yake kuwa mama yake alikuwa analala na Uncle kitandani huku wakiwa hawajavaa nguo. Hata hivyo mwanaume alipuuza kwasababu alikuwa anamuamini mke wake.

Siku hiyo baada ya mtoto kutoa siri hiyo, Ester alikataa kulala chumbani na mume wake na badala yake akadai anakwenda kulala chumbani kwa mfanyakazi wa ndani.

Ilipofika asubuhi mwanamke huyo alikutwa amejifungia chumbani na kujitoa uhai kwa kujining'iniza kwenye kitanzi.

Baada ya mwanaumehuyo kufanya uchunguzindipo alipobaini kuwa mke wake alikuwa ni 'Cha wote' na amefikia uamuzi huo kutokana na aibu ya kukutwa na mtoto wake akifanya mapenzi na mwanaume mwingine mbali na mume wake.