Friday, March 13, 2015

Taarifa Za Kufa Kwa Idadi Kubwa ya Wanafunzi Wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam katika ajali ya Iringa


 
Taarifa za awali kutoka vyanzo mbalimbali juu ya Ajali iliyotokea juzi kwa kuhusisha basi la kampuni ya Majinja yenye namba za usajili T438 CED na Lori lenye namba za usajili T 689 APJ, katika eneo la Changarawe, Mafinga Mkoani Iringa. Vilidai kuwa abiria wengi waliokufa katika ajali hiyo walikuwa ni wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam. 

Lakini kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi ameeleza kuwa miili ya abiria wengi ambayo inaendelea kutambuliwa walikuwa ni wafanya biashara wa eneo la Soweto, mjini Mbeya.

 Kamanda Mungi alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni ubovu wa barabara katika eneo la ajali na mwendo kasi. Baada ya magari hayo kugongana, Kontena lililokuwa limepakiwa katika lori hilo lilifyatuka na kudondokea basi hilo, hali iliyosababisha mauti na majeruhi wengi katika ajali hiyo.