Friday, March 13, 2015

IDADI YA WALIOFARIKI KWENYE AJALI IRINGA YAFIKA 50


 
Miili ya watu 8 tu kati ya 50 waliokufa kwa ajali ya juzi, iliyohusisha basi la kampuni ya Majinja yenye namba za usajili T438 CED na Lori lenye namba za usajili T 689 APJ, katika eneo la Changarawe, Mafinga Mkoani Iringa, ndiyo iliyotambuliwa mpaka kufikia jana mchana.

Idadi ya Marehemu hao iliongezeka kutoka 42 waliokufa mapema juzi hadi 50. Mmoja wa hao walio ongezeka aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa, ametambuliwa kwa majina ya Oswad Mwinuka (58)

Mganga Mkuu wa mkoa wa Iringa, Robert Salim alisema kati ya maiti 27 waliofikishwa hapo kutoka Mafinga ni wanane tu waliotambuliwa na ndugu zao, wengi wao kutoka jijini Mbeya.