Tuesday, March 10, 2015

ZITTO KABWE ANG'OLEWA RASMI CHADEMA


Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema), Tundu Lissu ametangaza kuvuliwa rasmi uanachama kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe.

 Baada ya Mahakama Kuu Tanzania kanda ya Dar es Salaam leo kutupilia mbali kesi iliyokuwa imefunguliwa na Zito Kabwe dhidi ya Chama Cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) ya kuhoji uhalali wa uanachama wake ndani ya chama hicho

Habari zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo Tundu Lissu ametangaza kuvuliwa rasmi uanachama wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe.

Akitangaza hatua hiyo ya kumvua uanachama,Lissu amesema kanuni na sharia za chama hicho ziko wazi na zinaelekeza kuwa endapo mwanachama yeyote atakishtaki chama hicho mahakamani na iwapo atashindwa atakuwa amejiondoa mwenyewe kwenye chama
    HABARI ZAIDI ZA KISIASA BOFYA HAPA>>