Wednesday, June 24, 2015

CCM YABARIKI UBUNGE WA MSANII WEMA SEPETU

Miss Tanzania 2006 na Staa wa Bongo Movie, Wema Sepetu akipokea maelekezo kutoka kwa katibu wa CCM wilaya ya Ikungi, Bw. Alluu Ismail Segamba kwenye Mkutano uliofanyika Mkoani Singida wiki iliyopita.



Siku chache baada ya mwanadada anayefanya vizuri kwenye filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ kutangaza nia ya kugombea ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), chama hicho kimempa baraka mrembo huyo kwa uamuzi wake huo.
…Wema akipokelewa na Makada wa Chama cha Mapinduzi, CCM mkoani  Singida.
Akistorisha na gazeti hili, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema kila mwanachama ana haki ya kugombea uongozi wowote ule ilimradi awe mwanachama hai, hivyo kwa Wema kugombea ubunge wa viti maalum ni haki yake na amefanya uamuzi sahihi.
“Kugombea uongozi ni haki ya kila mwanachama, Wema ana haki, kwanza ni mwanachama hai na baba yake alikuwa mwanachama mzuri sana wa CCM mpaka anafariki dunia, hivyo chama chetu huwa hakikutani na watu barabarani tu, bali wanakuwa ni halali kabisa mpaka wanatangaza kugombea,” alisema Nape.
Hata hivyo, alisema wasanii wote waliotangaza kugombea kupitia chama hicho hawajakurupuka bali ni wanachama hai na wamekuwa wakishiriki kwenye shughuli mbalimbali za kichama, tangu kwenye kampeni za mwaka 2010.
Wasanii wengine waliotangaza nia ya kugombea ubunge kupitia CCM licha ya Wema ni Ndumbagwe Misayo TheaĆ­ (Viti Maalum, Kinondoni) na Wastara Juma (Viti Maalum Morogoro Vijijini).