Wednesday, June 24, 2015

Msiba Mazito: Mbunge Afariki Dunia.

Mbunge wa Geita (CCM), Donald Max (58) amefariki Dunia katika Hospitali ya Taifa ya Nuhimbili (MNH) jijini Dar Es salaam.


Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema kuwa mbunge huyo (pichani chini) alifariki jana saa 12.00 jioni katika hospitali hiyo.
Ndugai alisema Max alikuwa mahututi kwa kipindi cha takribani miaka miwili iliyopita.
“Taratibu za maandalizi ya mazishi kwa sasa bado maana ni kama dakika 15 zilizopita ndiyo kafariki,” alisema Ndugai.
Max alizaliwa Mei 22 mwaka 1957 na kusoma katika Shule ya Msingi ya Salvatorian Convent na baadaye kujiunga na Shule ya Sekondari ya Azania mwaka 1971 hadi mwaka 1974.
Mwaka 1980 alikwenda nchini Urusi na kusoma kozi ya ufundi katika Chuo cha Ufundi cha Roston on Don kabla ya kujiunga na Taasisi ya Volgograd Polytechnical nchini humo na kutunukiwa Shahada ya Uzamili katika Uhandisi.