Picha hizo zitaendelea kuwa katika mtandao huo lakini hazitaorodheshwa katika
picha wakati wateja watakapozitafuta.
Makamu wa rais wa kampuni hiyo Amit Singhal amesema kuwa mpango huo
utashirikisha picha za uchi na zile zenye uchafu mkubwa.
Google hapo awali ilikataa jaribio la kuitaka kuondoa picha kama hizo katika
picha zilizoorodheshwa katika mashine yake ya utafutaji.
Mpango huo mpya unatarajiwa kuanza kufanya kazi katika kipindi cha wiki
chache zijazo.
Chanzo BBC