Sunday, June 21, 2015

Watu 90 Wafa Baada ya Kunywa Pombe yenye Sumu. BOFYA HAPA>>

Zaidi ya watu 90 wamefariki kutokana na pombe iliyokuwa na sumu katika mji wa India, Mumbai huku wengi wengine wakiwa Hospitalini.

Vifo vya kwanza viliripotiwa siku ya jumatano.

Naibu wa kamishna wa polisi katika mji huo amesema kuwa watu 150 waliokunywa pombe hiyo iliotengezwa nyumbani katika mtaa mmoja wa mabanda.
Vifo vinavyosababishwa na pombe ilio na sumu vimekuwa jambo la kawaida nchini India ambapo pombe rahisi inayotengezwa nyumbani ni maarufu miongoni mwa wakaazi wake walio maskini.
Chanzo: BBC