Wednesday, June 24, 2015

Serikali imeondoa Mswada wa sheria ya upatikanaji habari. HABARI KAMILI BOFYA HAPA>>

Hatimae Serikali imeondoa Mswada wa sheria ya upatikanaji habari wa mwaka 2015 bungeni ili kutoa fursa kwa wadau na kamati ya maendeleo ya jamii kuendelea kuujadili na kutoa maoni zaidi kwa lengo la kuboresha sheria.


Hatimae serikali imeundoa mswada wa sheria ya upatikanaji habari wa mwaka 2015 bungeni ili kutoa fursa kwa wadau na kamati ya maendeeo ya jamii kuendelea kuujadili na kutoa maoni zaidi kwa lengo la kuboresha sheria hiyo.

Akitoa taarifa ya serikali bungeni, waziri wa nchi ofisi ya rais asiye na wizara maalum, Prof Mark Mwandosya amesema serikali imetafakari maoni ya kamati na kuafiki mswada uendelee kufanyiwa kazi hadi kamati ya maendeleo ya jamii itakapokamilisha kazi yake na kuwasilisha maoni yake bungeni.

Wakati huohuo bunge limepitisha mswada wa sheria ya kuanzisha na kusimamia vituo vya pamoja mipakani wa mwaka 2015, ambapo akiwasilisha mswada huo, naibu waziri wa fedha Mhe.Adam Malima amesema lengo la sheria hiyo ni kuondoa changamoto zilizopo sasa za kukaguliwa mara mbili au zaidi kwa mizigo kwa ajili ya kukamilisha taratibu za forodha, ucheleweshwaji wa mizigo na kuvuja kwa mapato.