1. Kukiuka taratibu za chama kwaani alionekana kufanya kampeni badala ya
kutafuta wadhamini
2. Kutoa rushwa kwa wanachama mbalimbali hivyo kukigawa chama na kama angepishwa kuwa mgombea CCM ilikuwa katika hatari ya kuwekewa pingamizi mahakamani lakini pia angeweka watu wake kwenye utawala kuwalipa fadhira.
3. Edward Lowasa aliwahonga wajumbe katika uchaguzi wa wajumbe NEC uliofanyika
miaka iliyopita ili kupata watu wake ndani ya NEC.
4. Kuanza kampeni kabla ya wakati, alikuwa akisafirisha watu mbalimbali na kuwalipa fedha nyingi kisha kutoa taarifa kuwa walikuwa wakimtaka kugombea Urais, hii ni hadaa na hatari kwa chama.
5. Kuwa na kashfa nyingi za ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi ya umma akiwa waziri
6. Kusemwa semwa kuhusika kuhusika na tuhuma za kutumia watu kudhuru baadhi ya watanzania na viongozi, hili lipo kwenye vyombo vya dola kwa uchunguzi, uchunguzi ukikamilika sheria itachukua mkondo wake.
7. Utajiri na mali usiokuwa na maelezo alizipataje kama vile kumiliki majumba nje ya nchi kama uingereza, singapole na n.k
Mwisho chama kimesikitishwa sana na kauli kuwa amekuwa akionewa na kusingiziwa kuwa alihusika na kashfa ya RICHMOND, ndugu wanachama kashfa ya RICHMOND ilianzia bungeni,
CCM haikuhusika na kumwondoa kwenye uwaziri mkuu, lakini kwa kuwa imekuwa inajengeka kuwa alionewa tunaviomba vyombo vya sheria kulipeleka jambo hili mahakamani ili kuondoa dhana inayojengeka kuwa serikali ya CCM inaonea wanachama wake.
Doa linalotakwa kujengeka litapatiwa ufumbuzi na iwapo inathibitika kulikuwa na njama binafsi wote waliohusika kulidanganya bunge watachukuliwa hatua na chama lakini pia sheria itachukua mkondo wake
Imetolewa na :-
Nape M. Nnauye
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI.