Sunday, August 2, 2015

Majambazi yauwa walinzi wawili kwa kuwakatakata kwa mapanga Mkoani Mara


Watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wamewauwa kwa kukatwa katwa mapanga walinzi wawili wa kimasai ambao walikuwa wakilinda maduka katika eneo la Kiyara kata ya Kwangwa katika manispaa ya Musoma Mkoani Mara na kufanikiwa kupora vitu mbalimbali katika maduka hayo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara,kamishina msaidizi wa Jeshi la Polisi ACP.Ramadhan Ng’azi,amethibitisha kutokea kwa tukio hilo usiku wa kuamkia machi tisa mwaka huu na kusema kuwa Jeshi la  Polisi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja wa tukio hilo akiwa na baadhi ya vitu vilivyoibwa na kwamba upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kiyara Bw.Cosmas Majura na diwani wa kata hiyo Bw.Christopher Muyaga,wamesema vitendo vya ujambazi katika eneo hilo vinazidi kuongezeka kila kukicha kutokana na wananchi wake kutokukubali kushiriki katika mpango wa ulinzi shirikishi.