Chanzo chetu kimeshuhudia wanachama hao wakiongea kwa jazba huku
wengine wakinyanyua viti kupinga kitendo cha kurudia uchaguzi kwa mara ya pili
nakusema endapo watalazimishwa watakihama chama hicho na kwenda vyama vya
upinzani ambapo kikao kilivunjika na wajumbe wakaanza mzozo na mambo yalikuwa
hivi.
Aidha wanachama hao wameitaka viongozi CCM wilaya kutovuruga
matokeo hayo nakumtangaza aliyeshinda na vinginevyo wachague mwingine kati ya
watu watano waliogombea huku mwenyekiti wa kata Mussa Guzungwa ambae ndiye aliyeshinda
kura za maoni kugombea udiwani akijiuzulu na kuhamia vyama vya upinzani.
Naye katibu wa CCM kata ya Kimamba “A” Samweli Warioba
amesema tarifa hizo za malalamiko ya wanachama wamezipeleka kwa viongozi wa CCM
wilaya ya Kilosa na kwamba hawakubaliana na maamuzi ya kurudia uchaguzi.
Chanzo ITV